Mwenyekiti wa Bodi wa Busara Promotions, wandaaji wa tamasha la Sauti za Busara, Simai Mohammed (katikati) akiongea na wandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wanahabari Jijini Dar es Salaam, juu ya tamasha la 12 la Sauti za Busara, litakalofanyika, Februari 12 hadi 15, mwaka huu, Ngome Kongwe, Zanzibar. Wengine (kushoto) ni Meneja wa tamasha hilo, Journey Ramadhani. na upande wa kulia ni Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud ‘Dj Yusuf, akifuatiwa na msanii wa bongo fleva nchini, Ali Kiba (kulia). Msanii wa Bongo fleva nchini, Ali Kiba akiimba akapela moja ya nyimbo zake wakati wa mkutano huo na wandishi wa habari (Hawapo pichani), katika mkutano huo juu ya ushiriki wake kwenye tamasha hilo linalotarajia kufanyika Februari 12 hadi 15, Ngome Kongwe, Zanzibar. kushoto kwake, ni Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud ‘Dj Yusuf, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Busara Promotions, Simai Mohammed. Simai, Dj Yusuf na Kiba wakiwa wameunganisha mikono kwa...