Posts

Showing posts with the label MKUBWA NA WANAWE

Audio | Kayumba Ft. Aslay – MTOTO MBICHI | Mp3 Download

Image
Audio | Kayumba Ft. Asley – MTOTO MBICHI | Mp3 Download

Video mpya ya Mkubwa Na Wanawe(Yamoto Band) kuongozwa na GodFather wa Afrika Kusini.Diamond kaigaramia kila kitu.

Image
Muongozaji wa video za muziki wa Afrika Kusini, Godfather ataongoza video ya wimbo mpya wa kundi la Yamond Band ‘Cheza Kimadoido’ na Diamond ndiye atakayeigharamikia. Meneja wa kundi hilo, Said Fella, amesema Yamoto Band watasafiri Jumatatu kuelekea nchini Afrika Kusini kushoot video hiyo. “Wiki ijayo tunatarajia kufanya video mpya ya Yamoto Band na Godfather atakuwa director.Tuatashoot video hiyo Jumatatu,Jumanne na Jumatano maana bado tunashughuli nyingi.

YAMOTO BAND, MASHAUZI KUWASHA MOTO MANGO GARDEN LEO

Image
KWA mara ya kwanza baada ya miaka mingi, ukumbi wa Mango Garden, ulioko Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kupitisha wikiendi bila burudani yoyote, leo usiku ‘utawaka moto’ wakati Yamoto Band na Mashauzi Classic zitakapotoa shoo kabambe hapo. Wasanii wa yamoto band. Ni onyesho ambalo limeteka hisia za mashabiki wa muziki kutokana na ukweli kuwa vikundi hivyo viwili havijawahi kukutana katika katika onyesho la pamoja, ukiondoa yale matamasha yanayoshirikisha wasanii wengi. Kesho, Ijumaa,  Malaika Band ambao hupiga hapohapo Mango Garden, kila Ijumaa, watakuwa Arusha mjini wakitoa burudani. Mwimbaji na Kiongozi wa Kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’. Vilevile,  Twanga Pepeta ambao hupiga Mango Garden kila Jumamosi, wasanii hao Jumamosi hii watakuwa Wenge Garden Ukonga.  Bendi ya FM Academia ambayo huibuka Mango Garden na kufukia viraka vya bendi zilizopata dharura ya kuhama ukumbi, Ijumaa hii itakuwa Polisi Kilwa Road wakati Jumamosi itakuwa ...

Yamoto Band Kutua Mwanza kufanya yao kwenye mkesha wa Pasaka

Image
Katika kuikaribisha sikukuu ya pasaka wale vijana wanaojua kuitendea haki stage ya burudani Yamoto Band watakuwa jijini Mwanza wakimwaga burudani kwa wa wadau wa pande hizo husika.

Video :Yamoto Band wakizungumza na Charles Hilary katika BBC Dira ya Dunia

Image
Tazama hapa Yamoto Band walipokua wakizungumza na  Charles Hilary katika BBC Dira ya Dunia Nchini Londan

YAMOTO BAND KUKWEA PIPA TAREHE 17 KUELEKEA UK

Image
 Kundi la Muziki wa Kizazi kipya Yamoto Band wanatarajia kuanza safari yao ya kwenda UK kufanya Show tarehe 17 mwezi huu na show itapigwa Tarehe 21 ndani ya Royal Regency. Mkurugezi wa Kundi hilo Mkubwa Fella kwanza alianza kwa kutoa shukran zake kwa Mwenyezi Mungu, Mashabiki, Wadu na vyombo vyote vya habari kwa kuweza kutoa sapoti kwa vijana hao tangu walipo toa Kazi yao ya kwanza kabisa mpaka kufikia Leo wamepata mualiko mkubwa kabisa wa kwenda kufanya show UK, na kwa upande wa Msemaji mkuu na Kiongozi wa Band Aslay Isihaka amesema kuwa wanafuraha sana kwa kupata mualiko huo lakini pia wanashukuru kwa mungu, mashabiki na wale wote wanaonyesha sapoti katika muziki wao. Aslay amesema   kuwa watakwenda kufanya Kazi nzuri huko ili kuleta sifa ya muziki wa hapa nyumbani na hata heshima ya Taifa kwa ujumla.Kwa upande mwingine Vijana hao Wametoa shukrani zao kwa Viongozi wao Mkubwa Fella, Bab Tale, Chambuso, Mh Temba na Shirko kwa usimamizi Mzuri wa Kazi hizo.

Tazama hapa Picha za utengenezaji wa video mpya ya YAMOTO BAND “NITAKUPWELEPWETA”

Image
Leo tarehe 23 ndio ile video ya NITAKUPWELEPWETA inatoka rasmi ya wasanii hawa kutoka kundi la Mkubwa na Wanawe (Yamoto Band). Video imefanywa na kampuni ya Next Level chini ya Dir Adam Juma.

Yamoto Band wamalimalizia kushoot ‘Nitakupwelepweta’

Image
Yamoto Band wako kazini! Mwaka 2014 ni kama ulikuwa mwaka wao, tumezisikia kazi nzuri zilizopendwa kutoka kwao kwa kipindi cha mwaka mzima. 2015 wameanza kwa kurekodi video ya wimbo wao, kazi inafanywa Dar es Salaam na director Adam Juma.

Yamoto Band yauanza mwaka mpya na mashavu ya kimataifa, kwenda Uingereza mwezi wa pili

Image
djpaul620@gmail.com Bendi ya vijana wadogo inayokua kwa kasi kubwa Yamoto Band, imeuanza vizuri mwaka mpya kwa kupata show za kimataifa ikiwa ni mwaka mmoja tu toka itambulishwe rasmi. Meneja wa Yamoto, Said Fella ametoa ratiba ya bendi hiyo kwa mwaka huu (2015) , na miongoni mwa show wanazotarajia kufanya miezi ya mwanzoni ni pamoja na show ya Uingereza. Kupitia Instagram Fella aliandika: “Aya wadau napenda ya kuwafamisha ratiba ya mwaka huu ya moto band leo tar 1 leo daimond kawaalika rwanda tar 4 tupo maisha club kuzindua ngoma interview tar 10 tupo kigoma tar 31 watawasindikiza wakubwa zao mh temba, chege na madee kwenye utambulisho wa ngoma na video walofanya kaburu ukumbi wa escape 1 na tar 14 mwezi wa 2 watakuwepo musoma na tar 21 ndio MUNGU akipenda vijana watakuwa UK inshaallah MUNGU akipenda”.

Tazama Picha: Mkubwa na Wanawe yatoa msaada kwa kituo cha watoto yatima Temeke

Image
Katika kusherehekea kutimiza mwaka mmoja wa Yamoto Band, kituo cha Mkubwa na Wanawe leo kimekabidhi msaada kwenye kituo cha watoto yatima kilichopoa Temeke, Dar es Salaam. Akikabidhi msaada huo, mkuu wa kituo hicho, Said Fella alisema: Kabla ya kuzungumza chochote Napenda kutoa shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu kwa kila jambo ambalo limefanikiwa ni kwa kupitia yeye aliye muweza wa yote.” “Pili nawashukuru Watanzania wote karibu kila nyanja kwa kuonyesha ushirikiano wao kwa Mkubwa na Wanawe mpaka kufikia hapa hii leo.Toka ianzishwe Yamoto Band leo ni siku ya furaha kwetu kusheherekea mwaka mmoja ambao umefanyika kuwa na mafaanikio mengi makubwa. Moja kati ya mafanikio hayo ni kuuza kazi zetu kweye mtandao na kukuletea kokote ulipo mpaka majumbani,” alisema. Aliongeza: Na kwa hiki kidogo tulichokipata sisi ukijumuisha na furaha tuliyo nayo ya kutimiza mwaka mmoja tumeona ni bora tugawane na wenzetu ambao ni wahitaji haswa kwa msimu huu wa sikukuu kama tulivyozoea kufanya...