Baada ya Diamond kuweka wazi kuwa kituo cha runinga cha kimataifa, MTV Base huwa wanampigia kuidhinisha video yoyote inayotumwa kwenye kituo hicho kutoka Tanzania ili azitolee maoni kama zipitishwe ama laa, kauli hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti na wadau wakiwemo wasanii wenyewe. Miongoni mwa wasanii waliozungumza kuhusu kauli hiyo ni pamoja na Alikiba, ambaye itakumbukwa kuwa video zake hazioneshwi na kituo hicho, kitu kinacholeta sintofahamu pia kutokana na tofauti zake na Diamond. “Nitawaambia ukweli ambao unawahusu, kama ni kweli watakuwa wanakosea (MTV), haikai sawa na sidhani kama ni kweli,” alisema Alikiba kupitia 255 ya XXL alipoulizwa maoni yake kuhusu swala hilo. “Yaani haikai sawa na sidhani kama ni kweli, kwasababu watakuwa hawako fair, ndio hivyo hawako fair, hajabeba talent ya kila mtu (Diamond), kila mtu ana kipaji chake na kila mtu ana haki ya kuonesha kipaji chake kazi yake. Unajua kila mtu anafanya biashara ya muziki saizi, sio mtu anafanya masihara una...