Mwigizaji Wastara Azungumzia Mahusiano Yake Na Bondi.
Kwenye friday nite live ya eatv, mwigizaji Wastara amezungumzia mahusiano yake na mwigizaji maarufu wa filamu Tanzania “Bondi” nakusema “ Nikiwa karibu na mwanaume yeyote sasa watu huzusha maneno ila mimi na Bondi tunafanya kazi pamoja tu, ni manager wangu na husimamia kazi zangu, siwezi kufanya kila kitu mwenyewe ” Wastara yuko mbioni kuanza kufanya filamu mpya na kuanzia Januari 5 2014, atakuwa kambini.