Posts

Showing posts with the label NAY WA MITEGO

Nay wa Mitego na Diamond Platnumz wana mpango wa kuachia album yao ya pamoja

Image
Hivi karibuni, Nay alisema tayari yupo kwenye mazungumzo kuhusu mpango wa kufanya album hiyo. “Tumekuwa na mazungumzo nadhani tukifikia mwisho, tutakuwa na album ya pamoja mimi na Diamond. Kitu ambacho kipo tayari kwa sasa ni ujio wa tour yetu ya Mapenzi Pesa. Kwahiyo mashabiki wakae tayari kwa vitu vikubwa.”

Kaa Tayari; Dayna kuja na hii"Nitulize"akiwa na Nay.

Image
Dayna nyange anatarajia kudondosha mzigo mpya aliomshilikisha mkali wa Akadumba Nay wa Mitego.Kwa sasa mtarajia kumsikia Nay katika collabo nyingi za wasani wa kike,Kupitia instagram yake amepost picha na kuandia hivi: Ni moja kati ya collabo ambayo itafanya vizuri sana,Na nimeamua kufanya collabo na wasani wa kike kwa asiilimia 90% na 1 hii ni mwanaume alisema Nay. :

Haya ni maneno ya Ney Wa Mitego kuhusiana na collabo yake na Diamond Platinumz inayokujia hivi karibuni...

Image
Msaniii Nay wa Mitego ambae kwa sasa bado anahit na ngoma yake ya Akadumba amefunguka na kusema kuwa mashabiki wa Ney na Diamond Platnumz wakae mkao wa kula kwani mzigo wao mpya muda wowote ndani ya wiki hizi mbili unashuka, Nay wa Mitego amesema hayo na kusisitiza kuwa anadhani wimbo huo wa sasa huenda ukawa ni wimbo mkubwa kuliko wimbo wa awali waliotoa wakali hao unaofahamika kama Muziki gani. Nay wa Mitego amesema kuwa kutokana na matatizo yake ya kifamilia ndiyo yamechelewesha kukamilishwa kwa wimbo huo lakini kwa kuwa amesharudi na kutatua hayo matatizo hivyo ngoma inamaliziwa siku mbili hizi na kisha baada ya hapo mipango ikaa sawa siku yoyote ngoma hiyo itatoka ili kuwapa raha mashabiki zao. "Yeah kuhusu ngoma hiyo naweza kusema ipo tayari ingawa mimi kuna vitu kidogo bado sijavimalizia kutokana na ukweli kwamba siku mbili tatu zilizopita nilikuwa na matatizo ya kifamilia hivyo nilipata dharula nikasafiri na sasa nimerudi hivyo nitamalizia na kila kitu kikie...

Collabo ya Diamond Platnumz na Nay wa Mitego inatayarishshwa na Producer..

Image
Tudd Thomas ndiye producer atakaye simamia kazi mpya ya wasanii Diamond Platnumz na Nay wa Mitego, Walikesha usikuwa wa kuamkia 19 Feb 2015. Wimbo utafanyika Surround Studios.Hivi ndivyo alivyoandika Producer huyo kwenye instagram yake

Nay Wa Mitego na Diamond Platnumz studio tena,ni collabo nyingine

Image
Wasanii waliofanya #VituAmazing na wimbo wao wa Muziki Gani wamekutana tena studio kwaajili ya rekodi nyinine. Ni Diamond na Nay wa Mitego. Diamond kwa sasa anang’ara na rekodi ya Ntampata wapi ambayo inapewa muda mkubwa wa hewani kwenye vitui vya kimataifa ka Trace Tv huku Nay akifanya vizuri na rekodi na video ya Akadumba

Alichosema Ney Wa Mitego Kuhusu Nikki Mbishi Kuacha Muziki

Image
Kupitia exclusive interview na Power Jams, Ney wa Mitego amezungumzia hatua ya Nikki Mbishi ya kuacha muziki nakusema “ Ukiona kitu hakikulipi ni bora uachane nacho, mtu anaweza kuangalia kitu na kujua hakimfai na bora afanye mambo mengine ” Ney aliendelea kusema ” Sijui kwanini amechelewa, nimefurahi kuona maamuzi mazuri kijana mwenzangu aliyofanya, amejitambua na kuamua kuangalia vitu vingine, niko tayari kumshauri kama bado hajapata cha kufanya ” .

Video mbili za ‘Akadumba’ zimemkamua shilingi milioni 36 Nay wa Mitego

Image
Nay wa Mitego amekata mpunga mrefu kushoot video mbili tofauti za ngoma yake ‘Akadumba’ Nay amesema kuwa, shilingi milioni 36 zimetumika kukamilisha mzigo huo. “Kiukweli kabisa imenigharimu pesa nyingi sana ambayo sikufikiria kama inaweza ikanigharimu kiasi hicho,” amesema Nay. “Nilikuwa natafuta kitu kizuri na kuwaonyesha watu nini kinatufanya tutoke nje. Kwahiyo video moja nimefanyia nchini Kenya na Kelvin Bosco na moja nilimsafirisha akaja hapa nyumbani Tanzania, zote kafanya yeye. Kwahiyo zote zipo tayari. Zimegharimu zaidi ya milioni 36. Kwahiyo mpaka sasa hivi ninaweza nikasema zitatoka kabla mwaka huu haujaisha. Moja itatoka Alhamis ijayo ambayo nimefanyia nyumbani na hii nyingine itatoka mwaka huu huu.”