Video mbili za ‘Akadumba’ zimemkamua shilingi milioni 36 Nay wa Mitego
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Nay wa Mitego amekata mpunga mrefu kushoot video mbili tofauti za ngoma yake ‘Akadumba’
Nay amesema kuwa, shilingi milioni 36 zimetumika kukamilisha mzigo huo.
“Kiukweli kabisa imenigharimu pesa nyingi sana ambayo sikufikiria kama inaweza ikanigharimu kiasi hicho,” amesema Nay. “Nilikuwa natafuta kitu kizuri na kuwaonyesha watu nini kinatufanya tutoke nje. Kwahiyo video moja nimefanyia nchini Kenya na Kelvin Bosco na moja nilimsafirisha akaja hapa nyumbani Tanzania, zote kafanya yeye. Kwahiyo zote zipo tayari. Zimegharimu zaidi ya milioni 36. Kwahiyo mpaka sasa hivi ninaweza nikasema zitatoka kabla mwaka huu haujaisha. Moja itatoka Alhamis ijayo ambayo nimefanyia nyumbani na hii nyingine itatoka mwaka huu huu.”
Brand New Video From Raymond (Rayvanny) , The Song Is Titled Natafuta kiki (Official Video) .. Watch And Download Here... Enjoy DOWNLOAD MP4 WATCH FROM YOUTUBE