Posts

Showing posts with the label SHETA

Ngoma mpya ya Shetta akiwa kashirikiana na KCEE 'Shikorobo' kutoka kesho

Image
Kupitia account yake ya Instagram mwimbaji *Shetta* ameeleza namna alivyokuwa anaisubiri kwa hamu siku ya kuachilia ngoma hiyo. Ameandika haya "*Leo ni jumatatu tunashinda kesho Alafu ile jumatano sasa kesho kutwa tarehe 25/3/2015 mzigo huu ambao hata mimi nilikua nasubiri kwa hamu utoke ndio unatoka sasa utapata kusikia na kuona kwa macho yako nikimaanisha Video na Audio kwa pamoja.

Picha,Sheta anajitayarisha kutoa kitu kingine kikubwa Afrika.

Image
Sheta anajitayarisha kutoa video mpya hivi karibuni, kufuatia single yake ya Kerewa ft Diamond Platnumz iliyofanya vizuri Afrika kwa kuwa na video bora, Sheta ameonekana kuwa karibu na msanii Kcee huku pakiwa na uvumi kuwa anafanya naye kazi mpya inayotoka muda wowote sasa. Hizi ni baadhi ya picha kuhusu hii kazi mpya. Sheta na Kcee Sheta, GodFather na Kcee Sheta na phyno

Collabo kati ya Sheta na msanii Wa Nigeria Kcee inanukia soma hapo

Image
Ukizungumzia miongoni mwa wasanii wa Tanzania ambao nyimbo zao huchezwa hadi kuingia kwenye Top 10 za radio Nigeria basi Mkali wa hit single ya Kerewe, Sheta lazima awepo kwenye list yako. Shetta ambaye kwasasa yupo Afrika Kusini ameonekana akiwa na mkali wa hit single ya Limpopo,  Kcee  kwenye maandalizi ya video mpya lakini bado haijajulikana  video hiyo inayotengenezwa ni ya nani. Siku chache zilizopita kupitia instagram,  Kcee  alipost picha akiwa na Shetta na kuandika;… “Work mode: on set with my bro @Shettatz no time…”—- @ iam_kcee

Ndoa ya Sheta Yafikisha miaka miwili sasa

Image
Shetta na mke wake Leila wametimiza zaidi ya miaka miwili kwenye ndoa yao na rapper huyo amedai kuwa ni furaha tu ndio iliyotawala familia yake.Shetta na Leila walifunga ndoa mwaka 2012 na hadi sasa wamebarikiwa mtoto mmoja wa kike aitwaye Qayllah. Rapper huyo amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kumpa nguvu huku familia yake ikiwa ni yenye upendo na amani. “Mimi nilioa huko nyuma na matunda yake ndo haya unayaona, Qayllah. Nilioa lakini sikufanya sherehe, ilikuwa kimya kimya saa kumi na mbili baada ya watu kumaliza ile swala ya saa 11 ndo ikapita. Kwahiyo Mama Qayllah ni mke wangu wa ndoa. Sikupiga picha wala nini. Qayllah “Watu wengi hawakufahamu kwa sababu haikuwa na shamra shamra pia sikupenda kuweka wazi mambo yangu ya kifamilia kwa wakati huo. Lakini namshukuru Mungu mpaka sasa hivi nafurahia maisha yangu pamoja na familia yangu,” aliongeza Shetta.