Posts

Showing posts with the label KITAIFA

Majaliwa Amtumbua JIPU Mhandisi wa Maji Nyumbani Kwa Rais Magufuli

Image
Rungu la kuwatumbua majipu watumishi wa umma wasiowajibika limetua kwa Mhandisi wa Maji Wilaya ya Chato, Peter Ngolemi baada ya Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa kuagiza kusimamishwa na kuamuru Takukuru kumchunguza kutokana na kumdanganya.   Ngolemi, anadaiwa kumdanganya Majaliwa kuhusu mradi wa maji katika Kijiji cha Kalebezo ambao umesababisha wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.   Mradi huo umesimama tangu mwaka 2011, kutokana na kukosa usimamizi baada ya mashine mbili kutofanya kazi. Licha ya kumsimamisha, Waziri Mkuu aliagiza Takukuru kumchunguza na kumchukulia hatua za kisheria.   “Hatuwezi kuwa na kiongozi muongo, naondoka naye. Mtumishi huyu atakaa pembeni Takukuru wamchunguze,” alisema. Kabla ya kuchukua uamuzi huo, Majaliwa alimwita jukwaani na kumtaka ajibu madai ya wananchi kukosa maji muda mrefu. “Mheshimiwa Waziri Mkuu, kuna mashine mbili na hili suala lipo kwa Mamlaka ya Maji Bukoba, lakini zile pampu mbili zipo,” alijibu N...

Rais Magufuli Apiga MARUFUKU Kukodi Mitambo ya Kuzalisha Umeme

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 16 Machi, 2016 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi namba mbili, uliopo katika wilaya ya Ilala Mkoani Dar es salaam, ambao utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 240 za umeme.   Mradi huo ambao utazalisha umeme kwa kutumia gesi asilia inayosafirishwa kwa bomba kutoka Mtwara, unatarajiwa kuanza kuzalisha umeme katika kipindi cha kuanzia miezi 21 hadi 28 utakapokamilika kabisa.   Kuanza kwa ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme huo, kunafuatia juhudi zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano ya kufanikisha upatikanaji wa shilingi bilioni 120, ikiwa ni asilimia 15 ya fedha zilizopaswa kutolewa na Tanzania na fedha nyingine shilingi Bilioni 292 zimetolewa na Japan.   Mradi huu umetanguliwa na mradi wa Kinyerezi namba moja ambao una uwezo wa kuzalisha megawatts 150 za umeme, na mitambo yake tayari imeanza uzalishaji wa megawatts 105 z...

Rais Wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang Akaribishwa Ikulu, Jijini Dar Leo

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kushoto) akimkaribisha mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam. Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kulia) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye koti la drafti) mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam. Kulia niRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa tatu kulia) akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (wa tatu kushoto) mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya ku...

Wadaiwa 16 Waliotorosha Makontena Bandarimni Kuanza Kufilisiwa Leo

Image
Wadaiwa 16 waliokwepa kulipa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), baada ya kutorosha kontena za mizigo yao kwenye Bandari Kavu (ICD) ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, mali zao zinaanza kukamatwa leo na kufilisiwa. Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono, iliyopewa kazi ya kufuatilia wadaiwa hao wakiwemo baadhi ambao wamekamilisha malipo, Yono Kevella alisema hayo Dar es Salaam jana. Kevela alisema kuanzia leo wanakaa na vyombo vya dola, kuanza utaratibu wa kukamata na kufilisi mali za wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Kevela alisema hadi sasa hakuna zuio lililotolewa, linazowazuia kutekeleza wajibu wao katika kukusanya madeni hayo. Hata hivyo alisema, wengi wa wadaiwa baada ya kutolewa kwa muda huo wa siku 14, wameonesha moyo wa kulipa. Wadaiwa 16 hawajamaliza madeni Alitaja wadaiwa 16 ambao hawajalipa madeni yao wala kupunguza, ambao watafilisiwa wasipojitokeza kufanya malipo ni Said Ahmed Said Sh 28,249,352.50, Strauss International (4...

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AWASILI MKOANI SINGIDA

Image
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone wakati alipowasili mjini Singida tayari kwa maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM yanayotarajiwa kufanyika mjini Singida Jumamosi  Februari 6 mwaka huu kwenye uwanja wa michezo wa Namfua mkoani humo, wa pili kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na mkuu wa wilaya ya Singida mjini Mh. Said Amanzi. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kufanya Kazi” (PICHA NA JOHN BUKUKU – FULLSHANGWE-SINGIDA) Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo na Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone wakati alipowasili mjini Singida tayari kwa maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM yanayotarajiwa kufanyika mjini Singida Jumamosi  Februari 6 mwaka huu mkoani humo, kushoto ni Mh. Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM na Waziri wa Habari Utamadu...

ILEMELA YAWEKA MSIMAMO WAKE DHIDI YA WAFANYABIASHARA WA HOTEL NA NYUMBA ZA KULALA WAGENI

Image
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Wanga akitoa ufafanuzi kwa Wanahabari juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni. Wafanyabiashara wa Hotel na  Nyumba za Kulala Wageni katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, Wametakiwa kufanya  biashara zao kwa mjibu wa kanuni na sheria za biashara zao ikiwemo kulipa  ushuru na kodi mbalimbali kama ilivyoidhinishwa na Serikali. Kauli  hiyo imetolewa hii leo na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Wanga, katika Kikao  cha Viongozi wa Manispaa ya Ilemela na Wafanyabiashara hao, juu ya Ufafanuzi wa  Sheria ya Kodi ya Malazi, ambayo imeanza kukusanywa kwenye Hotel pamoja na  nyumba zote za kulala wageni. “Kama  una wajibu wa kulipa kodi Majengo, leseni ya biashara, mabango, ushuru wa  malazi, ushuru wa huduma na kodi nyingine zote zilizo kisheria, ni vyema  ukalipa bila kushurutishwa. Kutokufanya hivyo utatufanya twende kwenye ule  mkono mwingine a...

Rais Magufuli Amuongezea Mwaka Mmoja Mkuu wa Majeshi Jenerali David Mwamunyange...Afanya Uteuzi wa Makamanda Wengine wa JWTZ

Image
RAIS John Magufuli amemwongeza muda wa mwaka mmoja Mkuu wa  majeshi ya ulinzi nchini,Jenerali David Mwamunyange, ambaye alitakiwa kustaafu leo baada ya kutimiza umri  kwa mujibu wa katiba na sheria. Akizungumza na waandishi wa habari leo mapema kwenye Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyopo  Upanga jijini Dar es salaam,Jenerali Mwamunyange amesema leo alitakiwa kuungana na Brigedia wanne wa Jeshi la ulinzi nchini  pamoja na Meneja Jenerali  wawili  ambapo wote kwa  pamoja wamestaafu ndani ya Jeshi kwa mujibu wa sheria ya jeshi hilo. “Mimi mwenyewe ilikuwa nistaafu kazi leo tarehe 30 Januari 2016,lakini Rais na Amri Jeshi mkuu ameamua kunibakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka mmoja kuazia leo tarehe 30 januari,2016 hadi tarehe  31 Januari 2017,” amesema Jenerali Mwamunyange Jeneral Mwamunyage amesema sababu iliyomfanya Rais Magufuli kumwongezea mda huo imetokana na Rais kutopata mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo...

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MAWENZI MKOANI KILIMANJARO

Image
Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Majaliwa Kassim Majaliwa akiwasili Ikulu ndogo ya mjini Moshi. Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisalimiana na Waziri mkuu  Majaliwa. Waziri Mkuu  akislimiana na Mstahiki meya wa  Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya . Waziri mkuu akiwasili katika hosiptali  ya rufaa ya Mawenzi alipofanya ziara  ya  kushtukiza. Waziri mkuu akitizama chumba cha kupigia  pcha za mionzi (X Ray) katika hospitali  ya rufaa  ya Mawenzi. Waziri mkuu akiwa wodi ya watoto alipotembelea kujionea namna ambavyo  wagonjwa wanahudumiwa. Waziri mkuu Majaliwa akizungumza jambo na mganga  mkuu wa mkoa  wa Kilimanjaro, Dkt Mtumwa  Mwako. Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akitoa taarifa ya mkoa kwa Waziri  mkuu  Kassim Majaliwa. Wakuu wa wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika mkutano huo. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Vunjo , Mhe. James Mbatia walipokutana Ikulu nd...

Picha: Haya ndo baadhi ya matukio yaliojili leo Bungeni mjini Dodoma

Image
Spika wa Bunge Job Ndugai (kulia)  akimwapisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa  , bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.     Spika wa Bunge Job Ndugai (kulia)  akimwapisha Waziri wa  Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango, bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.   Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Dkt. Abdallah Possi akijibu maswali Bungeni Mjini Dodoma Januari 26, 2016.   Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama  akijibu swali Bungeni Mjini Dodoma Januari 26, 2016.   Wabunge wakisikiliza hoja mbalimbali bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.    Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde  akijibu maswali Bungeni Mjini Dodoma Januari 26, 2016.   Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akiji...