Video: Diamond ajibu mapigo ya wanaomchukia kwa video hii ‘sexy’ ya Zari akiwa kitandani
Wote tunafahamu kuwa uhusiano wake na Zari the Bosslady unapigwa vita vikali na TeamWema! Well, Wema Sepetu alishawahi kusema kuwa hana kinyongo kwa Diamond lakini hiyo haimaanishi kuwa jeshi lake la watu zaidi ya 560,000 Instagram lina mtazamo huo pia! Team Wema haitakuja kuipenda couple yenye nguvu zaidi Afrika Mashariki ‘Zarimond’. Hilo Diamond analijua pia na ndio maana jana aliamua kuitoa character yake ya ‘uswahili’ ‘ushari’ kwa kupost video akiwa chumbani kwake kwenye mjengo wake ambayo yeye anauita state house! Kwenye video hiyo ambayo unasikika wimbo maarufu wa kihindi ‘Kuchi Kuchi’, anaonekana Zari akiwa kajilaza kitandani na gauni jekundu la kulalia. Kwenye video ya kwanza, Diamond anawaonya ‘haters’ kwa kuandika: ‘Crazy Us …Tafta kopo Ujiandae Kutapika maana Ndimu Zishakuzoea…. #StateHouseByNight.” ‘I am taking you straight to state house,’ anasikika Diamond akiongea kwenye video hiyo. ‘I see my beautiful baby she is right there.’ Katika video ya pili, staa huyo a...