Akiwa msanii wa tano kuifanya SOPHIA ya msanii BEN POL, yeye anaitwa TONTO yeye ameimba kama wifi yake SOPHIA...... ikiwa ni baada ya AYLER na NAY LEE kuimba wakichukua uhusika wa SOPHIA
Prisons imeibana Azam FC na kuilazimisha sare ya bila bao kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, jana. Sare hiyo inaifanya Azam FC kufikisha pointi 46 sawa na Yanga ambayo inaendelea kubaki kileleni kutokana na ubora wa mabao ya kufunga na kufungwa (GD). Kwa upande wa mechi ilikuwa nzuri na yenye ushindani mkubwa kwa kuwa kila timu ilionekana ilikuwa imepania kushinda mchezo huo wa Ligi Kuu Bara. Prisons imefikisha pointi 32 sawa na Mwadui FC inayonolewa na kocha mwenye maneno mengi, Jamhuri Kihwelo.