YANGA imeendelea kuonyesha kuwa haitaki utani katika msimu huu wa 2015/16, hiyo ni kutokana na mazoezi ambayo timu hiyo imekuwa ikiyafanya lakini zaidi ni kuwa kikosi cha kwanza kipo kamili. Yanga itakutana na Mbeya City, kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara lakini tayari Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, ameshapata kikosi kitakachocheza mchezo huo na mbadala wa wale ambao watapata matatizo au kuwa nje ya uwanja kwa sababu yoyote ile. Katika mazoezi ya jana asubuhi kwenye Uwanja wa Boko, Beach Veteran nje kidogo ya Dar, kocha huyo alipanga vikosi viwili na kucheza kama mechi kati ya hivyo vyote kilikuwepo kimoja alichoonekana akikiandaa zaidi kwa kukipa mbinu nyingi. Kikosi kinachoaminika kuwa ni cha kwanza na kitaanza katika mchezo wa kesho kiliundwa na; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Vincent Bossou, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Deus Kaseke, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Simon Msuva. Kikos...