Alikiba amewaomba watanzania kumpigia kura Diamond anayewania tuzo ya BET zitakazofanyika, Juni 26 Los Angeles, Marekani. Wiki iliyopita Diamond alitangazwa kuwania tuzo ya BET kwa mara ya pili kwenye kipengele cha Best International Act: Africa akiwa ni msanii pekee kutoka Afrika Mashariki huku tuzo hiyo ikiwaniwa na wasanii wengine kama Wizkid, Yemi Alade, AKA, Cassper Nyovest, Black Koffie, MZVEE na Serge Beynaud. Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Alikiba aliwaomba watanzania wampigie kura Diamond kwenye tuzo anazoshiriki za BET na kusema kuwa yeye ndiye msanii pekee anayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo hivyo watanzania wampigie kura ili aweze kushinda. “Of course nawasupport wote ndiyo, vote for Diamond kwenye tuzo za BET kwa sababu yeye ndiyo anayetuwakilisha,” alisema Alikiba. Alikiba kwa sasa ni msanii aliye chini ya label ya Sony Music na wimbo wake mpya ‘Aje’ unafanya vizuri kwenye TV na Redio japo una siku tano...