Mabingwa wa soka Tanzania Bara na wawakilishi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga SC leo imefanikiwa kuitoa Cercle de Joachim ya Mauritius kwa jumla ya mabao 3-0, kufuatia ushindi wa 2-0 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo wa kwanza ilishinda bao 1-0. Alikuwa ni Amissi Joselyn Tambwe, mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi ambaye aliifungia Yanga bao la kwanza katika dakika ya tatu ya mchezo kwa kichwa akimalizia kwa uzuri krosi ya winga Simon Msuva. Yanga waliendelea kulishambuliwa lango la wapinzani wao lakini kukosekana kwa umakini wa washambuliji wao kuliwanyima magoli mengi zaidi. Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Yanga walikuwa na akiba ya bao 1-0. Kipindi cha pili Yanga waliingia na nguvu mpya na kufanikiwa kuongeza bao la pili lililofunga na Thaban Scara Kamusoko mnamo dakika ya 56 kwa shuti kali akiwa nje ya boksi, baada ya kuanzishiwa mpira wa adhabu na beki Mwinyi Hajji Mngwali. Kwa matokeo haya Yanga sasa itakutana na APR kutoka...